Road Carnage in Imenti
Kule Nkubu, Imenti kusini, wakaazi wa eneo hilo wameitaka serikali kuingilia kati na kuwawekea vizuizi vya kuthibiti mwendo wa kasi wa magari  katika soko la Nkubu. Hii ni baada ya kisa cha hivi punde, ambapo watoto watano waligongwa na gari wanne kati yao kutoka kwa familia moja, ambapo mmoja aliaga dunia. Wakaazi wa Nkubu wanasema kuwa eneo hilo limekuwa hatari kubwa zaidi kwa watu wanaojaribu kupitia eneo hilo, na wakataka hatua zichukuliwe kuthibiti hali hiyo. Ajali hiyo ilihusisha lori moja aina ya canter na gari moja la kibinafsi.
-------
Residents of Nkubu, Imenti south are now appealing to the government to intervene and help in the construction of road bumps along Nkubu market. This was after five children were knocked down 4 among them being from the same family. Residents say the area has since become a black spot and measures should be taken to avoid further damage.