Wabukala's Wife Dead
Mkewe askofu mkuu wa kanisa la kianglikana hapa nchini, dr. Eliud Wabukhala, atazikwa jumamosi hii, tarehe 11, septemba.marehemu mama Caren nakhumicha Wabukhala, ambaye alizirai jana  jioni kabla ya kuaga dunia, atazikwa nyumbani kwao huko butonge, katika dayosisi ya Bungoma. Tumepokea habari kwamba askofu dr. Wabukhala, tayari amepanga ibada ya wafu ifanyike alhamisi hii ya tarehe 9, katika kanisa la all saints cathedral, hapa Nairobi. Mama nahumicha alifariki wakati askofu Wabukhala akiwa katika uwanja wa ndege wa jomo kenyatta, akijiandaa kusafiri kwenda london, kuhudhuria kongamano.wakati huo huo, makamu wa rais Kalonzo Musyoka ametuma ris ala za rambi rambi wa jamaa ya askofu wabukala, kufuatia kifo cha mkewe nakhumicha. Makamu wa rais alielelezea masikitiko yake kwa kifio hicho, akimtaja marehemu mama nakhumicha kama mama aliyejitolea kuisaidia familia yake na kanisa lote la ACK, na hivyo kuendeleza neno la mwenyezi mungu.
-------
Caren Wabukhala, the wife of the Anglican archbishop Eliud Wabukhala is dead. Reports indicate that Caren collapsed at her residence along state house road and was rushed to the Nairobi hospital where she was pronounced dead on arrival. According to the Anglican church dean Stephen Njihia, Wabukhala learnt of his wife’s demise as he was on his way to London to attend a church conference. The body of the deceased is at the lee funeral home awaiting a memorial to be held on Thursday at the all saints cathedral.